Breaking News
Breaking News
Dark
Light

Serikali Yaondoa Tozo Gesi ya Magari

"Kuanzishwa kwa ushuru huu kutaathiri vibaya jitihada zetu za kuhamasisha matumizi ya gesi asilia, ambayo ni nishati safi na salama kwa mazingira."
June 27, 2024
by

Serikali ya Tanzania imeridhia ombi la kuondoa ushuru wa shilingi 382 uliokuwa umepangwa kuwekwa kwenye kila kilo ya gesi asilia inayotumika kwenye magari kuanzia mwaka ujao wa fedha 2024/25.

Ushuru huo umeondolewa kufuatia ushauri wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, ambayo ilieleza kuwa sekta ya gesi bado ni changa na inaendelea kukua taratibu, na hadi sasa haijaweza kutumika kikamilifu nchini kutokana na gharama za kufunga mfumo wa kutumia gesi pamoja na uhaba wa vituo vya kujazia gesi.

Wabunge wengi waliochangia hotuba ya Bajeti ya Serikali ya mwaka 2024/25 walipinga kuanzishwa kwa ushuru huo, wakisema kuwa unaenda kinyume na azma ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kuchagiza matumizi ya nishati safi nchini.

Soma:Magari Ya Serikali Kutembea Mwisho Saa 12

Mbunge mmoja alisema, “Kuanzishwa kwa ushuru huu kutaathiri vibaya jitihada zetu za kuhamasisha matumizi ya gesi asilia, ambayo ni nishati safi na salama kwa mazingira.”

Kamati ya Bajeti pia imeishauri Serikali kuondoa kodi kwenye vifaa vinavyotumika kuunganisha mfumo wa gesi ili kupunguza gharama za kusimika mfumo huo kwenye magari, ambazo kwa sasa zinakadiriwa kuwa kati ya shilingi milioni 2 na milioni 3.

Kiwango hiki kinachukuliwa kuwa kikubwa sana kwa wananchi wa kawaida, na kuondoa kodi hii kutasaidia kupunguza mzigo wa kifedha kwa wale wanaotaka kubadilisha magari yao kutumia gesi asilia.

Kwa hatua hii, Serikali inaonyesha dhamira yake ya kuendelea kusapoti sekta ya gesi na kuhakikisha inakuwa kwa kasi inayostahili, huku ikihakikisha nishati safi inapatikana kwa urahisi na bei nafuu kwa Watanzania wote.

Author

1 Comment

  1. I am no longer certain where you are getting your information, however great topic. I must spend some time studying more or understanding more. Thanks for excellent info I was on the lookout for this info for my mission.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Don't Miss

Tanzania’s Economy Remains Stable, Central Bank Reports

Tanzania’s economy is on steady ground, according to the latest

Nape Urges Media to Amplify 4Rs Philosophy

Minister for Information, Communication and Information Technology, Mr Nape Nnauye,