Breaking News
Breaking News
Dark
Light

Rais Samia Akutana na Papa Francis Vatican Italia

Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Februari 12, 2024 amekutana na Papa Francis jijini Vatican na kufanya naye mazungumzo.
February 12, 2024
by

Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Februari 12, 2024 amekutana na Papa Francis jijini Vatican na kufanya naye mazungumzo.

Viongozi hao wamejadiliana masuala mbalimbali, ikiwemo mchango wa Kanisa Katoliki katika uboreshaji wa huduma mbalimbali za kijamii hususani elimu, afya na misaada ya kijamii pamoja na ushirikiano wa kimataifa wa pande zote mbili kujitolea kukuza amani dunia.

Wakati huo huo, Rais Samia amekutana na Katibu Mkuu wa Vatican, Kadinali Pietro Parolin na viongozi wengine akiwemo Paul Richard Gallagher anayeshughulikia uhusiano wa Vatican na mataifa mbalimbali duniani.

Sambamba na hilo Baba mtakatifu Francis amemteua Padre Wilbroad Kibozi wa jimbo kuu Katoliki Dodoma kuwa Askofu msaidizi wa jimbo hilo kuanzia leo,kabla ya uteuzi huo Askofu Kibozi alikuwa makamu Gambera, mlezi na mwalimu wa Seminari kuu ya kitaifa ya familia takatifu-Mwendakulima iliyopo jimboni kahama

Author

4 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Don't Miss

Tour Operators Oppose Tanzanian Shilling Payments

Tour operators in Tanzania’s northern regions have expressed strong opposition

Hamas Open to Ceasefire, Rejects Trump-Led Proposal

Amid the rubble and heartbreak in Gaza, a fragile signal