Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Bw. Bernard Konga ameeleza kuhusu maboresho ya Kitita cha Mafao kwa wanachama leo 28, Februari , 2024 akizungumza na waandishi wa habari Dar Es Salaam .
Konga amesema Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umefanya umefanya maboresho ambayo utekelezaji wake utaanza rasmi Machi 1, 2024.
“Kitita cha mafao ni orodha ya huduma za matibabu ambazo zinatolewa kwa wanufaika wa NHIF na bei zake ambazo hutumika wakati wa malipo kwa madai ya watoa huduma za matibabu. Maboresho ya mwisho ya kitita cha mafao cha NHIF kinachotumika sasa yalifanyika Juni, 2016 takriban miaka nane iliyopita na hivyo kuwepo kwa umuhimu wa kufanya marejeo yake kutokana na sababu mbalimbali kama zinavyoanishwa kwenye taarifa hii,” amesema Konga.
Konga ametaja malengo ya maboresho ya kitita cha mafao kuwa ni kuboresha upatikanaji wa huduma bora kwa wanachama ikiwa ni pamoja na kuongeza huduma ambazo hazikuwepo awali, Kufanya maboresho ya huduma na gharama zake kwa kuzingatia maendeleo ya teknolojia na hali halisi ya bei katika soko na Kuwianisha Kitita cha Mafao na miongozo ya tiba iliyoboreshwa ili kuongeza ubora wa huduma zinazotolewa kwa wanufaika wa Mfuko.
Malengo mengine ni Kujumuisha maoni na mapendekezo mbalimbali ya Wadau, Kutekeleza ushauri wa Taarifa ya Mapendekezo ya Tathmini ya Uhai na Uendelevu wa Mfuko kwa kipindi kinachoishia tarehe 30 Juni, 2021 na Kuimarisha udhibiti katika mianya ya udanganyifu.
Konga ameeleza kuwa Mfuko ulianza zoezi la kufanya marejeo ya kitita kuanzia mwaka 2018, hata tenhivyo utekelezaji wa kitita kipya haukufanyika kutokana na uhitaji wa kuhusisha wadau zaidi ili kuwa na uelewa na maoni zaidi kuboresha kitita hicho.
Maboresho ya Kitita cha Mafao yamehusisha kufanyika kwa Tathmini ya Uhai na Uendelevu wa Mfuko na kutekeleza mapendekezo yake ambapo tathmini ya mwisho ilifanyika Juni, 2021 ambapo Kifungu Na 15.2 cha Mkataba baina ya Mfuko na Watoa Huduma kinautaka Mfuko kutoa notisi ya miezi mitatu (3) ya kusudio la kufanya maboresho katika kitita chake kabla ya kuanza kutumika.
Additional Source:Ministry of Health
What’s Taking place i’m new to this, I stumbled upon this I have found It absolutely useful and it has helped me out loads. I am hoping to contribute & help other customers like its aided me. Good job.