Dark
Light

Kuwa na cheo kusikufanye uwabudiwe-Dkt. Dotto Biteko

Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Nishati, Dkt. Dotto Biteko amewataka Viongozi na Wafanyakazi wa Sekta mbalimbali Nchini ikiwemo wa TANESCO kuacha kujiona fahari au kutaka kuabudiwa na kutukuzwa kwasababu ya nafasi na vyeo walivyonavyo kwakuwa vyeo hivyo sio vyao milele bali ni vya muda tu.
March 18, 2024
by

Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Nishati, Dkt. Dotto Biteko amewataka Viongozi na Wafanyakazi wa Sekta mbalimbali Nchini ikiwemo wa TANESCO kuacha kujiona fahari au kutaka kuabudiwa na kutukuzwa kwasababu ya nafasi na vyeo walivyonavyo kwakuwa vyeo hivyo sio vyao milele bali ni vya muda tu.

Akiongea katika Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi Wizara ya Nishati leo March 18, 2024 Jijini Mwanza amesema “Wewe kuwa Mtu wa TANESCO au Wizara ya Nishati unaonaje fahari kuabudiwa na kutukuzwa kwasababu ya cheo ambacho kwanza sio chako ni cha Watu, hivi vyeo vyote mlivyonavyo ikiwemo cha kwangu sio vya kwetu ni temporary kwa ajili ya ku-service wakati ule”

“Kwanini msijifanyie Marafiki kwa vyeo mlivyonavyo?, kwanini mnajitengenezea Maadui kwa vyeo mlivyonavyo?, unafanya TANESCO Shirika zuri la Nchi linaonekana baya la hovyo, akisimama Mtu wa TANESCO mahali popote Watu wanaanza kucheka utafikiri kasimama Comedian kwasababu ya sifa za Watu wa mule ndani”

“Kumpelekea Mtu nguzo mpaka akupe hela na Wananchi wapo wanaojua kushawishi, atakushawishi kwa haraka zake anakwambia nisaidie niwekee nguzo hapa haraka kuna milioni hii hapa, utaichukua hiyo milioni siku nguzo imesimama atakumbuka milioni yake na atakwenda kwa wengine atawaambia ‘wale Jamaa hawapeleki nguzo mpaka milioni, unahangaika hapa, Mimi nimemgonga milioni, mbona kesho yake hivi’ tunaonekana wote humu Wapiga dili”

“Kabla ya boti yetu haijazama tumtazame Yona amekaa upande gani?, mnafahamu habari ya Yona, boti ilikuwa inatikisika tumepanda na Mtu ambaye anataka kuzamisha boti yetu, achana na Yona boti ifike salama mwisho, Watu wa kufanya hiyo kazi ni nyinyi Baraza la Wafanyakazi muambieni ukweli hasa Sekta ambazo zinakutana na Wananchi moja kwa moja mathalani TANESCO”

3 Comments

  1. hello there and thanks in your info – I’ve certainly picked up anything new from proper here. I did then again experience several technical points the usage of this website, as I experienced to reload the site many instances previous to I may just get it to load correctly. I were thinking about in case your hosting is OK? Now not that I’m complaining, however sluggish loading circumstances times will often affect your placement in google and could damage your high-quality rating if ads and ***********|advertising|advertising|advertising and *********** with Adwords. Well I’m including this RSS to my e-mail and could glance out for much extra of your respective intriguing content. Make sure you replace this once more very soon..

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Don't Miss

Tanzania,Japan Commits To Support Domestic Farmers With 377BN Tsh

The United Republic of Tanzania and Japan have signed a

Makonda Found Guilty of Power Abuse

The Human Rights and Good Governance Commission (THBUB) has found