Breaking News
Breaking News
Dark
Light

LATRA Waita Wadau Kujadili Nauli Mpya za Mwendokasi

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) imepokea maombi ya kurejea nauli za mabasi yanayotoa huduma ya usafiri wa haraka
June 27, 2024
by

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) imepokea maombi ya kurejea nauli za mabasi yanayotoa huduma ya usafiri wa haraka kutoka kwa UDART ambayo inatoa huduma za mpito za usafiri wa Mabasi ya Haraka katika Jiji la Dar es Salaam kama ifuatavyo:

1. Nauli kwa Abiria Njia Kuu (Truck Route) = 1,000TZS

2. Nauli kwa Abiria Njia Lishi (Feeder Route) = 600TZS

3. Nauli kwa Abiria Kimara – Kibaha 1,200TZS

4. Nauli kwa Mwanafunzi = 200TZS

Kwa mujibu wa Kifungu cha 21 cha Sheria ya Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini Sura ya 413, Mamlaka inapaswa kupokea maoni ya wadau kabla ya kufikia uamuzi wa kuridhia viwango vya nauli kwa huduma zinazodhibitiwa na Mamlaka ikiwemo nauli za mabasi. Katika kulitekeleza hilo, Mamlaka imeandaa mkutano wa kupokea maoni ya wadau wa usafirishaji, ikiwa ni pamoja na watoa huduma, watumiaji wa huduma na wananchi kwa ujumla.

Soma:DART Imewsimamisha Kazi Madereva Waliopeleka Abiria Morocco Badala Ya Kimara

Mkutano huo utafanyika tarehe 03 Julai 2024 katika Ukumbi wa mikutano Arnaoutouglou, Jijini Dar es Salaam kuanzia saa 3.30 asubuhi. Kutokana na umuhimu wa mkutano huo, LATRA inawaalika wadau wa sekta ya barabara na wananchi kwa ujumla kushiriki bila kukosa katika mkutano huo muhimu.

Kwa watakaoshindwa kufika kwenye mkutano huo, wawasilishe maoni yao ya maandishi katika Ofisi ya Mkurugenzi Mkuu iliyopo katika Jengo la Mkandarasi, Tambukareli Dodoma na Ofisi za Mikoa za LATRA kabla ya tarehe 19 Julai, 2024. Aidha, maoni ya wadau yanaweza kutumwa kwa barua pepe kupitia anuani zifuatazo: info@latra.go.tz na dg@latra.go.tz

Author

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Don't Miss

Titanic ‘Door’ Prop That Kept Rose Alive Sells For $718,750

The floating piece of wood that kept Titanic’s Rose alive

Deadly Plane Crash in São Paulo Kills 61

A Plane crash in São Paulo, Brazil, has claimed the