Breaking News
Breaking News
Dark
Light

Vijana wa Mafunzo ya Uongozi Watakiwa Mabalozi wa Tanzania , Marekani

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Said Shaib Mussa akisisitiza jambo alipokuwa akiwaaga washiriki wa programu ya mafunzo ya uongozi kwa vijana(Mandela Washington Fellowship for Young African Leaders is the flagship program)yatakayofanyika nchini Marekani.
June 11, 2024
by

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Said Shaib Mussa amewaasa vijana waliochaguliwa kushiriki katika programu ya mafunzo ya uongozi kwa vijana maarufu kwa jina la “Mandela Washington Fellowship for Young African Leaders” kuwa mabalozi wazuri katika mafunzo hayo yanayotarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 18 Juni, 2024 jijini Washington, Marekani.

Nasaha hizo zimetolewa katika hafla fupi ya kuwaaga vijana hao 26 ambayo ilihusisha makabidhiano ya bendera ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwa ni ishara ya kuitangaza na kuiwakilisha nchi katika heshima inayostahili iliyofanyika katika Ofisi za Wizara Mtumba, Dodoma tarehe 10 Juni, 2024.

Balozi Mussa aliwapongeza vijana hao kwa kuonesha uwezo na jitihada binafsi kuchukua nafasi ya kuomba na kufanikiwa kupita katika mchujo wa vijana wengi walioihitaji fursa hiyo. Hivyo, ni wema wakazingatia mafunzo na kuhakikisha ujuzi na elimu watakayoipata inaleta manufaa kwao na kuwajengea uwezo vijana wengine waliopo nchini.

‘’ Hii ni programu maalum ambayo itawajengea uwezo katika masuala ya uongozi hususani, uongozi katika masuala ya usimamizi wa umma, uongozi katika usimamizi wa biashara na uongozi katika masuala ya ushirikishwaji wa jamii yakiwa ni maeneo mtambuka katika ukuaji wa nchi za Afrika,” alisema Balozi Mussa.

Soma:Bashungwa Awataka Vijana Kuacha Maisha ya Anasa

Pia akawaeleza umuhimu wa kuzingatia sheria na taratibu za nchi husika pamoja na kujikita katika malengo yanayowapeleka nchini Marekani ili kufanikisha kutumia fursa hiyo kujenga uwezo katika maoneo yao husika ya kiutendaji sambamba na kuijengea nchi sifa nzuri.

Aidha, amewasisitiza kuzingatia tamaduni na mila za kitanzania wawapo nchini humo kwakuwa mafunzo hayo yanahusisha mataifa tofauti hivyo ni vema kuepuka changamoto mbalimbalii za kimaadili zinazoweza kuwaharibia sifa binafsi na taifa kwa ujumla. Vilevile, katika hilo akasisitiza umuhimu wa kuwasilisha taarifa zao katika ofisi za ubalozi zilizopo jijini Washington.

Nao vijana wanaoenda kushiriki mafunzo hayo wameishukuru Serikali kwa kuendeleza kuimarisha ushirikiano mzuri na Serikali ya Marekani na hivyo kuwawezesha kushiriki kwa wingi katika mafunzo hayo ambayo pamoja na masuala mengine yatawajengea na kukuza uwezo katika teknolojia inayopatikana katika taifa hilo kubwa lililopiga hatua kimaendeleo sambamba na kukutana na wadau katika sekta husika.

Programu hii inatarajiwa kutimiza miaka 10 tangu ianzishwe mwaka 2014 ambapo imekuwa ikitoa mafunzo kwa washiriki kwa njia ya vitendo na kuingia darasani na hivyo, kuwawezesha kushiriki katika majukumu ya kijamii pamoja na kufanya ziara katika ofisi mbalimbali za umma na mashirika nchini Marekani.

Author

2 Comments

  1. I really enjoy looking at on this internet site, it has got excellent posts. “Dream no small dreams. They have no power to stir the souls of men.” by Victor Hugo.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Don't Miss

Tundu Lissu Becomes Chadema’s New Chairman

 Tundu Lissu has emerged victorious, replacing Freeman Mbowe as the

Peter Responds To Paul: “I Am Not Competing With Him”

Last Week, News Emerged About P-Square Breaking Up for the