Breaking News
Breaking News
Dark
Light

Unyanyasaji, ubaguzi kikwazo waandishi wa habari wa kike – Twaweza

Mkurugenzi wa utetezi kutoka taasisi ya TWAWEZA Annastazia Rugaba amesema wabahabari wa kike wanapitia changamoto nyingi katika utendaji wao wa kazi wakiwa kwenye vyombo vyao vya habari.
February 16, 2024
by

Mkurugenzi wa utetezi kutoka taasisi ya TWAWEZA Annastazia Rugaba amesema wabahabari wa kike wanapitia changamoto nyingi katika utendaji wao wa kazi wakiwa kwenye vyombo vyao vya habari.

Akitoa taarifa ya utafiti huo kwa waandishi wa habari leo Februari 16 jijini Dar es Salaam, Rugaba amesema waandishi wa kike wanakabiliwa na hali ya ubaguzi, unyanyasaji, mfumo dume, kutopewa nafasi za juu katika utendaji na malipo duni ya mshahara hali inayopelekea kupoteza ufanisi wa utendaji kazi wao.


Hata hiyo ametolea ufafanuzi wa harakati za kuwasaidia wanahabari wa kike ili kuondokana na changamoto wanazokutana nazo ikiwa pamoja na kutoa mafunzo kwa wanahabari hao kupitia wanahabari wakike wakongwe katika taslnia hiyo.
Sambamba na hayo Rugaba anaziomba mamlaka kuruhusu waandishi wa habari kutoa taarifa mbalimbali zinazotokea kwa manufaa ya taifa bila kuweka kipingamizi ikiwa ni moja ya hatua za kumlinda muandishi.
Pia amesisitiza uwepo wa mijadala mingi ya sekta ya habari ili kuboresha maisha,usalama na sheria bora ambazo zitakuwa rafiki na kukuza sekta hiyo kwakuwa inaumuhimu mkubwa kwa nchi na dunia kwa ujumla.

Author

2 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Don't Miss

Anti-Corruption Watchdog Blocks Ghost Grave Payout

Tanzania’s Prevention and Combating of Corruption Bureau (PCCB), known locally

Political will spurs dramatic drop in FGM practices

Political will has been mentioned as among the major helpful