Breaking News
Breaking News
Dark
Light

Sisi Tunahitaji Chama, Sera, Mgombea Urais Bora – Martine

Katibu wa idara ya uhusiano wa kimataifa vyuo na vyuo vikuu UVCCM Taifa Ndg Emanuel Martine akiwa katika mahafali ya UVCCM vyuo na vyuo vikuu Mkoa wa pwani amesema kuwa.
June 23, 2024
by

Katibu wa idara ya uhusiano wa kimataifa vyuo na vyuo vikuu UVCCM Taifa Ndg Emanuel Martine akiwa katika mahafali ya UVCCM vyuo na vyuo vikuu Mkoa wa pwani amesema kuwa. Tanzania inahitaji Mambo 3 pekee mwaka 2025 nayo yote yanapatikana ndani ya Chama cha Mapinduzi pekee amefafanua kuwa.

1. Chama: watanzania wote wanahitaji Chama ambacho ni Chama Bora, makini na chenye misingi thabiti isiyotetereka. Watanzania wanahitaji Chama cha Mapinduzi pekee kwani ni Chama chenye kutumainiwa na watanzania wote na ni Chama bora kwa watanzania wote chenye misingi thabiti isiyotetereka.


2. Sera: Chama cha Mapinduzi kinazo sera nzuri sana na zenye kupimika kwa watanzania wote, wanachama wa CCM na watanzania ni Wakati wetu kuzielewa Sera za CCM barabara na kuhakikisha tunaendelea kuziunga mkono Sera za CCM kwani ni muhimu kila mmoja ajue kuwa CCM pekee Tanzania ndiyo ina Sera za msingi Katika sekta zote na sera hizo zinapimika.

Soma:CCM Moto Umewaka, Makalla Aapa Kukitetea CHama.

3. Mgombea Urais Bora na mtulivu sana na mwenye upendo na Tanzania: watanzania mwaka 2025 hatuna budi kuendelea kumuunga mkono Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DKT SAMIA SULUHU HASSAN kwani yeye ni mama, ni mama mwenye upendo na watanzania wote bila kujali vyama vya siasa, Mhe Rais Fkt SAMIA SULUHU HASSAN ni kiongozi mahiri, shupavu, jasiri na mpenda maendeleo kwa Taifa letu la Tanzania, tuendelee kumuunga mkono na kama watanzania ni lazima wote tumuunge mkono kuijenga Tanzania, tusimame na Dkt SAMIA SULUHU HASSAN.

Hayo yamesemwa na kuelezwa na Katibu wa idara ya uhusiano wa kimataifa vyuo na vyuo vikuu UVCCM Taifa
Ndg Emanuel Martine mbele ya mgeni Rasmi Mhe Ridhiwani kikwete ambaye alikuwa anamwakilisha Rais mstaafu wa awamu ya nne Mhe jakaya mrisho kikwete Katika mahafali ya UVCCM vyuo na vyuo vikuu Mkoa wa pwani.

Author

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Don't Miss

Vijana wa Mafunzo ya Uongozi Watakiwa Mabalozi wa Tanzania , Marekani

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano

Afya ya Akili Inavyo Watesa Watu

Katika miaka ya hivi karibuni, afya ya akili imeibuka kama