Dark
Light

Radi kukwamisha shughuli za uchumi Njombe, Biteko atoa neno

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko amekemea uzembe unaofanywa na baadhi ya watumishi wanaochelewesha huduma kwa wananchi ikiwemo kubadili transfoma zinazopigwa radi hasa katika mkoa wa Njombe.
February 23, 2024
by

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko amekemea uzembe unaofanywa na baadhi ya watumishi wanaochelewesha huduma kwa wananchi ikiwemo kubadili transfoma zinazopigwa radi hasa katika mkoa wa Njombe.

Kauli hiyo ya Dkt. Biteko ameitoa katika ziara yake katika mkoa wa Njombe jimbo la Wanging’ombe kufuatia changamoto iliyowasilishwa na mbunge wa jimbo la Wanging’ombe ambaye ni Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt. Festo Dugange ambaye amesema mkoa wa Njombe unachangamoto ya radi ambazo zinapiga transfoma na kusababisha mgao hivyo kukwamisha shughuli za uchumi kwa wananchi wa mkoa wa Njombe hususan ni Wanging’ombe.

“Tunachangamoto kubwa ya radi kwa mwaka tunaweza kubadilisha transfoma 50,60 na kuendelea na mara nyingi transfoma ikiharibika inachukua miezi kadhaa umeme kuja kwa wananchi hii inaleta kero tunaomba transfoma zinanoweza kuhimili geografia Wanging’ombe na mkoa mzima wa Njombe “. Amesema Dkt. Dugange

Akijibu hilo Dkt. Biteko amesema “mbunge amesema transfoma ikiungua inachukua mwezi mmoja kubadilishwa uzembe huo hatuukubali na pale Tanesco makao makuu kuna watu walishazoea matatizo haiwezekani transfoma inaungua hakafu inachukua mwezi mzima ndio maana idara ya manunuzi pale Tanesco niliwambia wawabadilishe “. Amesema Dkt. Biteko

2 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Don't Miss

Rais Mwinyi akutana na Naibu Kamishna Wa Haki za Binadamu

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein

Polisi Mkoani Arusha kutoa huduma kidigitali

Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Mkoa wa Arusha SACP Justine