Breaking News
Breaking News
Dark
Light

Hakuna Sheria Kuwakamata Wanaokula Mchana-CP Hamad

“Shida iliyojitokeza operesheni hii ilikamata waliomo na wasiokuwemo, wavuta bangi na waliokula hadharani, Mampaka nyingine za Kiserikali huwa zinafanya oparesheni hiyo ya wanaokula mchana na wajibu wetu ni kusimamia ili ili zifanyike kwa salama na amani”
April 2, 2024
by

Jeshi la Polisi limekiri kutokua na uhalali wa kisheria wa kuwakamata watu wanaokula mchana huku akisema kuwa katika operesheni iliyofanyika hivi karibuni ilihusisha watu wanaovuta bangi jambo ambalo ni kinyume na sheria

Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar CP Hamad Khamis Hamad ameeleza hayo mbele ya waandishi wa habari ofisini kwake Ziwani Mjini Unguja

Amesema huenda kanuni nyengine zinatumika na mamlaka nyengine za kiserikali lakini kwa jeshi la Polisi hawana sheria inayowapa uwezo wa kuwakamata watu wanakula mchana wa Ramadhan hadharani kutokuwepo kwa sheria inayowapa nafasi ya Jeshi kuwakamata wanaokula mchana wa Ramadhan hadharani

“Hakuna sheri inayokataza Watu wasile mchana wa Ramadhani, nilitoa maelekezo baada ya video ya wanaovuta bangi kwamba ifanyike oparesheni wale wavuta bangi kwasababu bangi ni kosa la jinai hakuna sheria inayoruhusu Watu kuvuta bangi ila hatukuwakamata wala mchana”

“Shida iliyojitokeza operesheni hii ilikamata waliomo na wasiokuwemo, wavuta bangi na waliokula hadharani, Mampaka nyingine za Kiserikali huwa zinafanya oparesheni hiyo ya wanaokula mchana na wajibu wetu ni kusimamia ili ili zifanyike kwa salama na amani”

Aidha amesema tukio lilosambaa kwenye mitandao limewaonyesha watu mbalimbali wakiwa wanavuta bangi jambo ambalo ni kosa la jinai hivyo operesheni hiyo iliyofanyika na kuwakamata baadhi ya wahusika wa matukio hayo

“Nilitumiwa kipande cha video na kiongozi ambaye sitaweza kumtaja hapa ikionesha vijana wanavuta bangi na bahati nzuri yule mtu aliyekuwa anarekodi alikuwa anaongea,kuwa vijana wanavuta bangi mchana hapa,wanakula na vitu kama hivyo”
Ameongezea kuwa huenda zikatumika kanuni na taratibu nyengine na mamlaka nyengine za kiserikali hivyo jukumu lao ni kuhakikisha operesheni zinazofanyika zinakua salama bila kuleta athari kwa watu wengine

Read >>http://Tour Company Fined for Public Eating,Police Arrest 12 for Daylight Eating,

Sambamba na hilo CP Hamad amekumbushia matukio mbalimbali ambayo yanafanywa na taasisi zingine tofauti na polisi yamekuwa ni hatari kwasababu ya kukosa usalama kutoka kwa jeshi hilo.

“Mnakumbuka kuna tukio moja la taasisi fulani lilihusisha kuwakamata masaai baadae mliona kilichotokea, kwasababu walifanya operesheini yao bila kuwa na jeshi la polisi au usalama” amesema CP Hamad

Author

6 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Don't Miss

Ushirikiano Wilaya Malinyi ni Mbaya Sana – RC Malima

Watendaji wa Halmashauri Mkoani Morogoro wametakiwa kuwa mahiri katika kuzuia

TLS commits to assist poor citizens

The Tanganyika Law Society (TLS) has committed to assist poor