Dark
Light

Drum Beats Carnival Wasaini Mkataba na Wizara ,Tamasha La Utamaduni

Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Nicholas Mkapa (kushoto) akisaini Mkataba wa Ushirikiano na Bw. Mwesiga Selestine ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Drum Beats Carnival Tanzania Limited kuhusu ushirikiano katika uendeshaji wa Tamasha la Kitaifa la Utamaduni ambalo hufanyika kila mwaka nchini.
March 25, 2024
by

Halfla hiyo imefanyika Machi 25, 2024 katika Ofisi za Wizara Mtumba Jijini Dodoma na kushuhudiwa na baadhi ya Viongozi wa Wizara hiyo.

Akizungumza mara baada ya kusaini Mkataba huo, Naibu Katibu Mkuu Mkapa amesema Mkataba huo ni mwanzo mzuri wa kushirikiana na Sekta binafsi katika kuendesha matamasha ya wizara hiyo pia kupanua wigo kwa wadau wa sekta binafsi kushiriki kikamilifu katika uendeshaji wa matukio ya kijamii.

Kwa upande wake mwakilishi wa Kampuni hiyo Bw. Mwesiga amesema Kampuni hiyo itahakiksha Tamasha hilo linafanyika kwa ufanisi na kukidhi mahitaji ya wizara katika kutoa furaha kwa watanzania.

Tamasha la tatu la Utamaduni linatarajiwa kufanyika mwezi Agosti, 2024 Mkoani Ruvuma.

Author

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Don't Miss

Tabora United Cleared by FIFA After Settling Player Debts

The International Football Federation (FIFA) has lifted the ban on

Tanzania, Ghana business owners keen to increase trade engagement

SMALL scale business owners in Tanzania and Ghana have expressed