Wakala wa mabasi yaendao haraka (DART) imewasimamisha kazi watumishi wake sita baada ya kutokea vurugu kati ya abiria na madereva mnamo tarehe 26 machi 2024 majira ya saa nne usiku baada ya kuwapeleka abiria kituo kisicho sahihi.
Taarifa iliyotolea leo 28 Machi 2024 na DART imewasimamisha Shabani Kajiru-msimamizi wa kituo cha Kivukoni,Brown Mlawa – Afisa Ufuatiliaji kwa kushindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo ili kupisha uchunguzi wa kina.
Pia imemuagiza mtoa Huduma wa Mpito (UDART) Kuwachukulia hatua madereva Salehe Maziku, Chande Likotimo ambao walikuwa wanaendesha Basi kwa siku hiyo, msimamizi wa kituo hiko Lameck Kapufi na Afisa Usafirishaji Erick Mukaro ili kupisha uchunguzi wa kina.
Vilevile DART imetoa onyo kwa watumishi wake kuwa hawatosita kuwachukulia hatua endapo watakiuka maadili kwa watumiaji wa Mabasi yaendayo haraka.