Breaking News
Breaking News
Dark
Light

Aliyetakiwa Kuvunjiwa Nyumba Arusha Akubali Kumlipa Mwenzie

Hillary alipewa muda wa kukaa chini na Victoria ili wakubaliane kabla ya kuchukuliwa hatua za kuvunjiwa nyumba aliyojenga kwa mwenzake iwapo angekaidi
March 29, 2024
by

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Jerry Silaa amefanikiwa kumaliza mgogoro wa wakazi wawili ambao ni Victoria Chiwangu na Hillary Temu wa jijini Arusha ambao hapo awali Hillary alijenga kwenye kiwanja cha Victoria namba 313 Kitalu F Njiro, Arusha.

Hillary alipewa muda wa kukaa chini na Victoria ili wakubaliane kabla ya kuchukuliwa hatua za kuvunjiwa nyumba aliyojenga kwa mwenzake iwapo angekaidi.

Hata hivyo Hillary alikubali kumlipa Victoria kwa awamu na tayari ameisha mlipa sehemu ya fedha.

Waziri Silaa amemaliza mgogoro huo kwa kuwakutanisha wakazi hao katika Kliniki ya Ardhi iliyofanyika jijini Arusha ambapo hapo awali Waziri Silaa aliahidi kwenda kusimamia uvunjaji wa nyumba ya Hillary Temu.

Wakazi hao walikuwa na miaka 13 hawajasalimiana wala kushikana mikono, jambo ambalo Waziri Silaa alilimaliza kwa kuwapatanisha ndani ya dakika chache.

Author

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Don't Miss

201,707 Teachers to Undergo Recruitment Interviews in Tanzania

The Minister of State in the President’s Office for Public

Arusha Welcomes 2024 with Community Celebration

 Arusha residents flocked to the iconic Clock Tower junction to