Dark
Light

Waislamu Walia Na Bei Wakati Wa Sikukuu

Somoe Mshamu kutoka mtaa wa Salasala ameeleza Media Wire Express Kuhusu ongezeko la bei za bidhaa na vyakula madukani wakati huu wa sikukuu
April 9, 2024
by

Waumini wa dini ya kiislamu wanatarajia kusherehekea sikukuu ya eid Fitri siku ya jumatano na alhamis, baadhi yao wameeleza faida za mwezi huo pia kupanda bei za vyakula na bidhaa wakati wa Sikukuu hiyo.

Somoe Mshamu kutoka mtaa wa Salasala ameeleza Media Wire Express Kuhusu ongezeko la bei za bidhaa na vyakula madukani wakati huu wa sikukuu.

“Ukienda masokoni bei zimekuwa tofauti ukienda kununua nyama ilikuwa elfu nane (8,000) utakuta imepanda hadi elfu kumi (10)”

Pia amezungumzia kubadilika kwa maadili baada ya kuisha mwezi wa Ramadhani kwasababu ulikuwa na mafunzo.

” Mwezi wa Ramadhan ulikuwa wenye mafunzo na uadilifu kwa watu wengi lakini unapoisha hali ya tabia mbaya zitarudi kama awali, umewafanya watu wajistiri hasa wanawake waliokuwa wanavaa nguo za hovyo kuvaa vizuri hata watotowalikuwa wanaogopa kutukanakwasababu wamefunga” Somoe Mshamu

Pia tulizungumza na mfanyabiashara wa nyama ya ng’ombe kutoka Salasala ndugu Mussa  kuhusu  kupanda kwa bei ya nyama wakati huu wa sikukuu.

“Kupanda kwa bei ya nyama inatokana na machinjioni kupandisha bei, sisi tunaenda kutokana na kule wanakochinja”

kwa upande wake  Hussein Ramadhan amezungumzia uwepo wa Ramadhani na kuondoka kwake kuna mafunzo makubwa kwa waumini wa kiislamu.

“Ujio wa Ramadhani imekuwa na baraka naMwenyezi Mungu alitaka mwezi usiishe , pia  amewataka vijana na waumini wa dini ya kiislamu kudumisha yale waliyoyapata katika mwezi wa ramadhan na kusherehekea kwa wema.”

Pia amewakumbusha waumini wengine kutumia elimu ya mwezi huo kama sehemu ya malezi kwa watoto na familia kwasababu kuna mafunzo mengi yamepatikana kipindi chote.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Don't Miss

U.S. Tariff Hike on China Sparks Global Concerns

The United States has announced a significant increase in tariffs

Almayew Breaks Steeplechase Record at U20s

Sembo Almayew from Ethiopia captured the gold medal in the