Dark
Light

DART Imewsimamisha Kazi Madereva Waliopeleka Abiria Morocco Badala Ya Kimara

Mtoa Huduma wa Mpito (UDART) Kuwachukulia hatua madereva Salehe Maziku, Chande Likotimo ambao walikuwa wanaendesha Basi kwa siku hiyo, msimamizi wa kituo hiko Lameck Kapufi na Afisa Usafirishaji Erick Mukaro ili kupisha uchunguzi wa kina.
March 28, 2024
by
Wakala wa mabasi yaendao haraka (DART) imewasimamisha kazi watumishi wake sita baada ya kutokea vurugu kati ya abiria na madereva mnamo tarehe 26 machi 2024 majira ya saa nne usiku baada ya kuwapeleka abiria kituo kisicho sahihi.
 
Taarifa iliyotolea leo 28 Machi 2024 na DART imewasimamisha Shabani Kajiru-msimamizi wa kituo cha Kivukoni,Brown Mlawa – Afisa Ufuatiliaji kwa kushindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo ili kupisha uchunguzi wa kina.
 
Pia imemuagiza mtoa Huduma wa Mpito (UDART) Kuwachukulia hatua madereva Salehe Maziku, Chande Likotimo ambao walikuwa wanaendesha Basi kwa siku hiyo, msimamizi wa kituo hiko Lameck Kapufi na Afisa Usafirishaji Erick Mukaro ili kupisha uchunguzi wa kina.
 
Vilevile DART imetoa onyo kwa watumishi wake kuwa hawatosita kuwachukulia hatua endapo watakiuka maadili kwa watumiaji wa Mabasi yaendayo haraka.

Author

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Don't Miss

Rais Samia Azindua Tume Ya Ulinzi Binafsi

Rais Samia Suluhu Hassan amezindua Tume ya Ulinzi wa Taarifa

Air Tanzania Struggles with Rising Debt and Financial Woes

Air Tanzania, the national carrier, is facing significant financial challenges,