Breaking News
Breaking News
Dark
Light

Mabasi Yagonga Lori La Mafuta,Yawaka Moto

Mabasi mawili ya abiria moja likiwa mali ya kampuni ya Sauli luxury Bus linalofanya safari zake Dar es Salaam hadi Mbeya na lingine mali ya kampuni ya New Force enterprises limited yamegonga Lori la mafuta lililokuwa limeegeshwa pembezoni mwa barabara eneo la Ruvu barabara kuu ya Morogoro - Dar es Salaam.
March 28, 2024
by

Mabasi mawili ya abiria moja likiwa mali ya kampuni ya Sauli luxury Bus linalofanya safari zake Dar es Salaam hadi Mbeya na lingine mali ya kampuni ya New Force enterprises limited yamegonga Lori la mafuta lililokuwa limeegeshwa pembezoni mwa barabara eneo la Ruvu barabara kuu ya Morogoro – Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo Muda mchache kabla ya ajali, lory hilo la mafuta liliharibika barabarani kabla ya basi la kampuni ya Bm coach kulipita gari jingine baadae dereva wa basi la Sauli kulifuata basi hilo bila kuchukua tahadhari jambo lililopelekea basi la New Force kufuata nyuma.

Shuhuda huyo anaendelea kueleza kuwa basi la Sauli liliparamia lori hilo lililokuwa pembezoni mwa barabara kabla ya basi la New Force kuligonga basi la Sauli kwa nyuma kisha kuwaka moto Mda mfupi baadae.

Bado hakuna taarifa rasmi kutoka jeshi la polisi juu ya tukio hilo la mapema leo asubuhi.

 

Author

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Don't Miss

Why Putin’s Name Sends Shivers in Western Allies

The mere mention of the name Vladimir Putin sends a

Asilimia 20 ya samaki Ziwa Victoria wana plastiki

Wakati ulimwengu ukiadhimisha Siku ya Mazingira Duniani imeelezwa kuwa asilimia