Breaking News
Breaking News
Dark
Light

Vyakula vilivyoletwa na Marekani ni salama-TBS

Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limesema Mchele, Mafuta ya kupikia ya Alizeti na Maharage ambavyo vimeongezwa Virutubisho vilivyotolewa na Wizara ya Kilimo ya Marekani kwa ushirikiano na Taasisi ya Jumuiya za Kimataifa (Global Communities) kwa baadhi ya Shule za Dodoma, vyote ni salama kwa Walaji
March 18, 2024
by

Taarifa hiyo ya TBS imesema taratibu za uingizwaji wa chakula Nchini zilifuatwa ikiwemo ukaguzi na uchunguzi wa Kimaabara

Meneja Uhusiano na Masoko wa TBS, Gladness Kaseka amesema “Utaratibu wa kuongeza virutubisho kwenye chakula (food fortification) unakubalika kitaalamu na hufanyika kwa lengo la kuboresha hali ya lishe kwa walaji.”

Aidha shirk hilo limesisitiza litaendelea kuhakikisha chakula kinachoingia nchini kinakidhi vigezo vya usalama na bora kwa mujibu wa matakwa ya viwango ili kuendelea kulinda afya ya walaji.

Sambamba na hilo Siku chache zilizopita Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe alisema Taasisi hiyo ya Marekani inunue vyakula kutoka kwa Wakulima wa Tanzania na Virutubisho viwekwe huku Watanzania wakishuhudia.

Author

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Don't Miss

Tanzania ranked second least corrupt in EAC

Tanzania is the second least corrupt country in the East

63 Yr-old Man Killed By Unknown Assailants In Songwe Region

63 year old Kiminya Sambo, a resident of Nambizo Village