Breaking News
Breaking News
Dark
Light

Tanzania kuzalisha malighafi za injini za Ndege na Nyuklia

Waziri wa Madini, Mhe Anthony Mavunde amefanya ziara ya kutembelea sehemu ya eneo la mradi uchimbaji madini Tembo iliyopo katika kijiji cha Stahabu, Kata ya Mikinguni Wilayani Pangani Mkoani Tanga leo tarehe 20 Februari na, 2024 .
February 21, 2024
by

Waziri wa Madini, Mhe Anthony Mavunde amefanya ziara ya kutembelea sehemu ya eneo la mradi uchimbaji madini Tembo iliyopo katika kijiji cha Stahabu, Kata ya Mikinguni Wilayani Pangani Mkoani Tanga leo tarehe 20 Februari na, 2024 .

“Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameelekeza Wizara ya Madini kuhakikisha tunawezesha uanzishwaji wa miradi hii mikubwa na ya kimkakati ambayo itapelekea si tu ustawi wa uchumi wa Nchi yetu, bali kuwa kichocheo cha maendeleo na ustawi wa Wilaya ya Pangani na wananchi wanaozunguka mradi huu” amesema Mavunde.

“Amesema ni dhamira ya Serikali kuona wawekezaji wakubwa wenye nia njema na nchi ya Tanzania wanapewa ushirikiano ili kuwezesha shughuli zao kwa manufaa ya Taifa”.

Mradi huo unatarajiwa kuwa na thamani ya dola za kimarekani milioni 125 ambao uhai wake unakadiriwa kuishi kwa miaka 20 hadi 25 utatekelezwa katika Vijiji 8 vilivyopo katika Kata za Mikinguni, Mwera, Tungamaa na Bweni-Wilaya ya Handeni,Mkoani Tanga.

“Nimefurahishwa na utayari wa wananchi wanaoguswa na mradi kupisha kuanza kwa mradi, na kwa kuwa ni hatua muhimu sana kwani itarahisisha kuanza mradi kwa wakati na kuondoa changamoto ya migogoro kati ya wananchi na mwekezaji,” amesema Mavunde.

Akizungumza kwa niaba ya Mwekezaji, Mkurugenzi wa Kampuni ya Nyati Mineral Sand Ltd ambaye anawakilisha Hisa za Serikali, Heri Gombera amesa kwamba mradi huo unatarajiwa kuanza mwaka 2026 na unatarajiwa kuzalisha tani milioni 8 za madini mbalimbali kwa mwaka yakiwemo titanium, ilmenite, rutile, zircon na monazite ambayo pamoja na matumizi mengine hutumika pia kuzalisha malighafi za injini za ndege, nyuklia,vifaa vya hospitali na
viwanda vya marumaru na rangi.

Author

4 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Don't Miss

Tanzania Agencies Unite to Boost Revenue Collection

Four major Tanzanian government agencies have agreed to form a

ACT-Wazalendo Unveils Visionary Manifesto for Tanzania

ACT-Wazalendo, one of Tanzania’s leading opposition parties, has unveiled an