Breaking News
Breaking News
Dark
Light

Frateri Aliyejinyonga Azikwa Kimya Kimya

May 26, 2024
by

Ni siku chache zimepita baada ya  kuenea kwa taarifa ya kujinyonga kwa Frateri Rogassuan Massawe aliyedaiwa kujinyonga baada ya kufeli mtihani wa kumvusha daraja moja kwenda jingine katika masomo ya u padre , mwili wake umeweza kupumzishwa huku mamia ya watu wakijitokeza kumzika Frateri huyo { Rogassian Massawe], katika hgali isiyo ya kawaida mama yake mzazi, Levina Hugo ameshindwa kuhudhuria maziko hayo.

Frateri huyo ambaye amezikwa jana Jumamosi Mei 25, 2024 nyumbani kwao katika Kijiji cha Umbwe Onana wilayani Moshi Mkoa wa Kilimanjaro, anadaiwa kujinyonga Mei 20, 2024 kwa kutumia mshipi akiwa kwenye nyumba yao ya malezi ya Magambo iliyoko wilayani Lushoto mkoani Tanga.

Soma Zaidi:Askofu Ajinyonga Chanzo Ni Madeni

Inadaiwa, kabla ya kujinyonga Frateri Massawe aliandika ujumbe wa maandishi kwenye karatasi na kuuacha mezani ukisema; “Mama usilie, nimeshindwa kufikia malengo, ninajua nimewakwaza wengi.”

Hata hivyo, Frateri huyo wa Shirika la Roho Mtakatifu la Kanisa Katoliki, amezikwa bila kufuata taratibu za Kikatoliki, ambazo haziruhusu mtu aliyejinyonga kusomewa ibada ya maziko.

Akizungumza katika maziko hayo, Paroko wa Parokia ya Utukufu wa Msalaba, Jimbo Katoliki la Moshi, Anicet Alipenda amewaomba waombolezaji kuiombea familia ya Frateri huyo kwa kuwa mama yake mzazi Levina bado amelazwa hospitalini kutokana na mshtuko alioupata baada ya kupokea taarifa za kifo hicho.

Author

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Don't Miss

Tanzania Strengthens Diplomatic Ties with Finland Visit

Tanzania’s diplomatic landscape continues to evolve, with recent efforts reflecting

ECOWAS Envoy Faye To Broker Sahel Crisis Talks

West Africa’s fractured regional bloc on Sunday urged Senegalese President