Breaking News
Breaking News
Dark
Light

Vijana Watakiwa Kuchangamkia Fursa Mbadala

Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa amewataka vijana nchini kuchangamkia fursa zilizopo katika sekta mbalimbali ikiwepo ya Madini kama ajira mbadala
May 19, 2024
by

Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa amewataka vijana nchini kuchangamkia fursa zilizopo katika sekta mbalimbali ikiwepo ya Madini kama ajira mbadala na namna ya kujikwamua kiuchumi wao binafsi na familia zao sambamba na kuongeza mchango wao katika maendeleo ya taifa kwa ujumla.

Dkt Kiruswa amesema hayo Wilayani Longido Mkoani Arusha wakati akizungumza katika Kongamano la Vijana wilayani humo, ambalo limelenga kuwasaidia vijana kufahamu fursa zilizopo katika sekta za madini, kilimo, ufugaji pamoja na mikopo ya Halmashauri kwa Vikundi ya Wanawake, Vijana na Walemavu.

Dkt. Kiruswa amesema, kutokana na changamoto zilizopo katika soko la ajira hivi sasa ulimwenguni kote, ni wakati wa vijana kuhamisha fikra na nguvu zao katika ajira mbadala na kwamba fursa zilizopo katika Sekta mbalimbali kama vile Programu ya Mining for a Brighter Tomorrow (MBT) pamoja na Sekta Binafsi zinatoa nafasi kwa vijana wenye elimu na waliyokosa fursa za kusoma kufikia vyuo vya kati na vyuo vikuu.

“Mataminio ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kuona vijana wanachamgamkia fursa za ajira mbadala ili kunufaika na fursa mbalimbali zilizopo katika sekta binafsi na ametuelekeza kuwasadia vijana kufahamu fursa hizo na kuwawezesha kimbinu pamoja na mitaji kufikia ndoto zao” amesema Dkt. Kiruswa.

Soma Zaidi: DC Kibaha Awapa Somo Vijana Namna Yakujikwamua Kiuchumi

Aidha, Dkt. Kiruswa amewataka vijana kuunda vikundi ili wanufaike na mikopo ya asilimia 10 ya Halmashauri kwa ajili ya Vikundi vya Wanawake, Vijana na Walemavu ili kujikwamua kiuchumi kwa kuwa Serikali imeshafanyia marekebisho namna ya usimamizi wa mikopo hiyo na mwaka ujao wa fedha itaanza kutolewa kwa vikundi hivyo.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Longido Mhe. Marko Ng’umbi amewataka vijana kuzingatia mafunzo na maarifa waliyoyapata kwenye kongamano hilo na kuyafanyia kazi kwa kuwa ni fursa ya kipekee kwao itakayowasaidia kuwafungua kifikra na hatimaye kujiajiri.

Author

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Don't Miss

India Weighs Cutting Tariffs on US Imports

India is quietly considering a bold economic move: slashing tariffs

CHRAGG Dismisses Human Rights Violation Claims

The Commission for Human Rights and Good Governance (CHRAGG) has