Breaking News
Breaking News
Dark
Light

Tanzania Kunufaika Nishati ya EAPP, SAPP

Tanzania inatarajiwa kunufaika na uanachama wake katika jumuiya za nishati za Afrika Mashariki yaani (East African Power Pool) na Kusini (South Africa Power Pool)
May 14, 2024
by

Tanzania inatarajiwa kunufaika na uanachama wake katika jumuiya za nishati za Afrika Mashariki yaani (East African Power Pool) na Kusini (South Africa Power Pool) katika maeneo mbalimbali ikiwemo biashara ya umeme pamoja na kuunganishwa katika gridi ya pamoja.

Hayo yamebainishwa na Naibu Mkurugenzi mtendaji usafirishaji umeme Mhandisi Abubakar Issa katika warsha ya siku tano iliyowakutanisha wakuu wa sekta ya nishati pamoja na washauri kutoka nchi 13 Afrika, kujadili na kupanga mikakati mbalimbali ya namna ya kuunda kanuni za soko la nishati ya katika biashara ya kuuziana umeme kwenye kanda hizo.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi mtendaji kutoka TANESCO Naibu Mkurugenzi mtendaji Mhandisi Abubakar Issa amesema Tanzania ni mwanachama wa Jumuiya za nishati za ukanda wa Afrika Mashariki (EAPP) na kusini mwa Afrika (SAPP) ambazo lengo lake ni kuwezesha upatikanaji wa umeme wa uhakika katika nchi hizo kwa kuangalia biashara ya kuuziana umeme na uwepo wa gridi ya pamoja.

Soma Zaidi:TANESCO: “Umeme Umekatika Baada Ya Hitilafu Gridi Ya Taifa”

“Tanzania tutakuwa na uwezo wa kuuza au kununua umeme katika jumuiya za nishati za Afrika Mashariki na Kusini. Kitendo cha miundombinu yetu itakapokuwa imeunganisha jumuiya zote mbili, tutafaidika na mapato kama nchi. Na hii pia itasaidia kuhakikisha nchi zote za Afrika zinasaidiana katika kuwa na umeme wa uhakika. Hili litakuza uchumi wa Tanzania pamoja na bara letu kwa ujumla kwakuwa umeme ni uchumi” amesema Mhandisi Issa.

Ameongeza kuwa miundombinu inaendelea kuunganishwa na malengo ni kwamba biashara ianze mara tu muunganiko wa miundombinu hiyo itakapokamilika.

“Tunaunganisha ukanda wa Mashariki na Kusini mwa Afrika mfano sisi na Kenya tayari na kwa sasa hivi tunaendelea na Zambia ambapo kwa upande wa Tanzania tuko tayari, na tutakuwa tayari zaidi pale miundombinu inayoendelea kujengwa itakapokamilika,” ameongeza. Issa.

Author

4 Comments

  1. Hi, i think that i noticed you visited my website so i got here to “go back the prefer”.I am trying to find issues to enhance my website!I assume its adequate to make use of a few of your ideas!!

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Don't Miss

PSSSF tasked to intensify education on service provision

All agencies under the Prime Minister’s Office have been assigned

Nchi Wanachama Kukuza Amani Na Usalama Afrika

Katika maadhimisho ya kuadhimisha miaka 20 tangu kuanzishwa kwa Baraza