Naibu Karibu Mkuu Wizara ya Tamisemi anaeyeshughulikia Elimu Dkt. Charles Msonde amewataka walimu kutumia moja ya Kanuni za kuchunguza uwezo wa mwanafunzi na kutumia nyezo zitakazomwezesha mwanafunzi huyo kuelewa vizuri masomo badala ya kuharakisha kumaliza mada (Topics).
Dkt. Msonde amesema hayo wakati akizungumza na walimu wa shule mbalimbali za Halmashauri ya wilaya ya Mbogwe katika amesema ni heri mwanafunzi akafundishwa na kuelewa vizuri hata mada (Topics) 15 kuliko kumharakisha kufundisha ili umalize mada (Topics) 20 na mwanafunzi kutoelewa itakuwa ni kazi bure.
Kwa upande mwingine Dkt. Msonde amewaomba walimu kuendelea kujivunia kuwa katika fani ya ualimu kwakuwa wamepewa kibali cha kumsaidia Mh. Rais Samia Suluhu Hassan katika nyaja ya elimu waendelee kujivunia hilo wakati Serikali ikiendelea kutatua changamoto za malimbikizo ya mishahara,ajira za walimu na maboresho ya madaraja zaidi ya walimu Elfu 54.
Soma Zaidi:Biteko awashukuru walimu Bukombe kwa kuongeza ufaulu
Wakati akitoka taarifa ya divisheni ya elimu msingi na sekondari kwa Halmashauri ya wilaya ya Mbogwe Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Jummane Yassin amesema halmashauri hiyo ina jumla ya shule 103 za msingi na sekondari ambapo idadi ya jumla ya wanafunzi wa shule za msingi ni 90,467 na kwa upande wa shule za sekondari ni 13,502.
Baadhi ya walimu wa halmashauri ya wilaya ya Mbogwe wametoa pongezi zao kwa Naibu Katibu Mkuu Tamisemi Elimu Dkt. Charles Msonde kushuka kuzungumza na walimu hao kwa mifano halisi ya ualimu na kwa hakika kila mmoja aliyesikia atahakikisha watafanyia kazi maelezo yaliyotolewa.
It is really a nice and helpful piece of info. I’m happy that you shared this helpful info with us. Please stay us informed like this. Thank you for sharing.
You could certainly see your enthusiasm in the work you write. The world hopes for more passionate writers like you who aren’t afraid to say how they believe. Always follow your heart.
It’s impressive that you are getting thoughts from this piece of writing as
well as from our dialogue made here.
Perfect work you have done, this internet site is really cool with excellent information.
naturally like your web-site but you need to check the spelling on several of your posts. A number of them are rife with spelling issues and I find it very troublesome to tell the truth nevertheless I will definitely come back again.