Breaking News
Breaking News
Dark
Light

Watanzania Kufuata Ushauri wa Madaktari Matumizi ya Dawa

Serikali imeendelea kuboresha huduma za afya kwa watoto wachanga, ambapo idadi ya hospitali zenye wodi maalum za watoto wachanga (NCU) imeongezeka kutoka 14 mwaka 2018 hadi 241 mwaka 2024.
May 22, 2024
by

Mhe. Ummy Mwalimu, ametoa wito kwa Watanzania kuacha kujitimizia matumizi holela ya dawa bila kufuata ushauri wa madaktari.

Hii ni hatua muhimu katika kupambana na tatizo la usugu wa dawa dhidi ya vimelea, ambapo dawa hizo husumbuka kuponya. Akizungumza katika Semina ya Afya iliyofanyika Tanga, Waziri Ummy ameeleza umuhimu wa kufuata ushauri wa madaktari wakati wanapoagiza dawa na kutoa maelekezo kuhusu matumizi yake. Hii itasaidia kuzuia tatizo la usugu wa dawa, ambalo husababisha dawa kushindwa kuponya magonjwa.

Aidhan  Ummy amewakumbusha wajawazito kuhudhuria kliniki mapema pindi wanapohisi ujauzito, ili kupunguza vifo vinavyohusiana na uzazi. Pia, amewasisitiza wajawazito kujifungulia katika vituo vya kutolea huduma za afya, ili kuepuka vifo vya watoto wachanga.

SomaZaidi;Madhara Yakutumia Dawa Za Kuongeza Makalio

Serikali imeendelea kuboresha huduma za afya kwa watoto wachanga, ambapo idadi ya hospitali zenye wodi maalum za watoto wachanga (NCU) imeongezeka kutoka 14 mwaka 2018 hadi 241 mwaka 2024.

Katika semina hiyo, kulijadiliwa mada mbalimbali za afya, ikiwa ni pamoja na elimu kuhusu mifumo ya afya, afya ya uzazi, mama na mtoto, na ushiriki wa wanaume katika afya ya uzazi pamoja na wajibu wa jamii nzima katika kupunguza vifo vya watoto wachanga wanaozaliwa na uzito pungufu.

Author

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Don't Miss

Rwanda Accused of Supporting M23 Rebels Amid Denials

A recent report by United Nations experts has brought renewed

Father Accused of Brutal Murder of Infant Daughter

A man is facing charges of sexual assault and murder