Breaking News
Breaking News
Dark
Light

Mapambano Dhidi ya Wanyamapori Wakali

Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Uhifadhi wa Maliasili kwa Jamii (CBCTC) Likuyu Sekamaganga, Bi Jane Nyau, alibainisha kuwa kati ya askari 136 walioanza mafunzo, askari 135 waliohitimu mafunzo kati yao 108 ni wa kozi ya VGS na 27 ni wahitimu wa kozi ya muda mfupi
June 8, 2024
by

WaharWizara ya Maliasili na Utalii imeendeleza mkakati thabiti wa kupambana na wanyamapori wakali na waharibifu na kuimarisha uhifadhi kwa kutoa mafunzo kwa Askari Wanyamapori wa Vijiji (VGS) 135.

Katika hafla ya kufunga mafunzo hayo iliyofanyika katika Chuo Cha Mafunzo ya Uhifadhi wa Maliasili kwa Jamii (CBCTC) Likuyu Sekamaganga, Mkoa wa Ruvuma, Kanali Ahmed Abbas Ahmed ameeleza kuwa utoaji wa mafunzo hayo kwa VGS ni sehemu ya jitihada za serikali chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Ahmed aliwahimiza wahitimu kuyatimiza mafunzo waliyopata kwa weledi ili kuchangia katika kulinda wananchi dhidi ya wanyamapori wakali na waharibifu, kuendeleza uhifadhi wa rasilimali, na kuimarisha sekta ya utalii nchini.

Kwa upande wa askari wahitimu 27 wa utalii na uongozaji watalii, aliwataka kufanyakazi kwa weledi katika maeneo yao kwa lengo la kukuza utalii wa ndani na wa kimataifa.

SomaZaidi;Askari Wapya Watakiwa Kuenzi Maadili, Ataka Ubunifu FITI

Akizungumzia mipango ya wizara katika kuboresha mazingira ya utoaji elimu katika chuo hicho, Mkurugenzi wa Kitengo cha Utafiti na Mafunzo, Dkt. Edward Kohi, alisema wizara imeandaa mpango wa kuwapatia mafunzo watumishi wa chuo hicho katika ngazi mbalimbali za elimu na kuhakikisha kinakuwa na kituo cha afya.

Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Uhifadhi wa Maliasili kwa Jamii (CBCTC) Likuyu Sekamaganga, Bi Jane Nyau, alibainisha kuwa kati ya askari 136 walioanza mafunzo, askari 135 waliohitimu mafunzo kati yao 108 ni wa kozi ya VGS na 27 ni wahitimu wa kozi ya muda mfupi ya utalii na uongozaji watalii, huku askari mmoja akishindwa kuhitimu kutokana na utovu wa nidhamu.

Bi Nyau aliongeza kuwa mafunzo hayo yamedhaminiwa na Mradi wa REGROW, Shirika la GITZ, na Shirika la WCS.

Author

7 Comments

  1. Please let me know if you’re looking for a writer for your blog. You have some really great posts and I think I would be a good asset. If you ever want to take some of the load off, I’d really like to write some articles for your blog in exchange for a link back to mine. Please shoot me an e-mail if interested. Cheers!

  2. Thank you, I’ve just been looking for information approximately this subject for a while and yours is the greatest I have discovered so far. But, what concerning the bottom line? Are you certain in regards to the source?

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Don't Miss

Tanzania Prepares For Vuli Rainfall October 2025

Tanzania is preparing for the October–December 2025 Vuli rainfall season,

Kenya Faces Job Losses Without AGOA Extension

Kenya’s textile industry is bracing for a potential crisis as