Breaking News
Breaking News
Dark
Light

Makonda: Tayari Kupoteza Chochote Kwa Maslahi Ya Wananchi

Makonda ameyasema hayo leo wakati akizungumza na  wananchi waliojitokeza kwenye kliniki ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi.
May 8, 2024
by

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda, amewaambia wananchi wa mkoa huo kwamba yupo tayari kupoteza chochote alichonacho ili mwananchi mmoja wa Arusha aweze kupata haki yake na kunufaika na cheo chake.

Makonda ameyasema hayo leo wakati akizungumza na  wananchi waliojitokeza kwenye kliniki ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi.

Read More:Makonda Aogopa “Kuyakoroga” Mbele ya Makamu wa Rais

Amesema hawezi kukaa kwenye kiti cha mkuu wa mkoa ilihali wananchi anaowaongoza wakiteseka na changamoto mbalimbali ambazo zipo ndani ya mamlaka yake ya uongozi.

Aidha, Makonda amewataka wananchi hao kung’ang’ana kudai haki yao wasiogope kwa kuwa Rais Samia Suluhu Hassan, ametoa wanasheria bingwa kutoka ofisi zaidi ya 75 za mawakili ili kuwasikiliza na  kuwapa misaada ya kisheria.

Makonda amesema hatokubali kuendelea kuona vilio vya wana Arusha waliokata tamaa kutokana na kutosikilizwa kero zao na kutatuliwa akiahidi kuijenga heshima yake kwa kurejesha haki kwa wananchi wa Arusha walionyang’anywa haki zao.

Makonda aliyeteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan Takribani Mwezi mmoja uliopita kutoka kuwa katibu mwenezi wa  itikadi CCM kuwa mkuu wa mkoa wa Arusha amekuwa akiwahimiza mara kadhaa watendaji mbali mbali na viongozi wengine wa serikali kuwa wachapakazi kwa manufaa ya wananchi wa mkoa huo.

Author

2 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Don't Miss

Kenyan Catholic bishops react after Pope authorized blessings for same-sex couples

Kenya Conference of Catholic Bishops (KCCB) has come out to

Mamelodi Sundowns Bring Own Provisions Amid Sabotage Concerns

Yanga’s opponents in the CAF Champions League quarterfinals, South African