Dunia Imekumbwa na Aina Mpya Ya Urembo Kwa Wanawake, Urembo Wa Kuongeza Makalio ili Kuwa Na Muonekano Bora Zaidi.
Oktoba 27,2023,Hospitali Ya Taifa Ya Muhimbili-Mloganzila, ilianza Rasmi Huduma ya Upasuaji Wa Kupunguza Uzito na Upasuaji Rekebishi Yaani (Bariatric And Reconstructive Surgery) Ambapo Upasuaji Huo Unahusisha Kurekebisha Maungo,Ikiwemo Kupunguza Au Kuongeza Ukubwa wa Tumbo,Matiti Na Makalio.
More On: Fahamu madhara ya kuongeza makalio
https://www.mwananchi.co.tz/mw/
Idadi Ya Wanawake Wengi Wenye Kwenda Na Fasheni Na Kupendezesha Miili Yao, Wamejitupa Katika Dimbwi la Kutumia Vidonge Mbali Mbali Kama Njia Mbadala Tofauti na Njia Ya Upasuaji iliyopendekezwa na Kushauriwa Na Madaktari na Kuangukia Katika Madhara Makubwa kama Kansa na Miili Yao Kuwa Na Umbile Lisilo la Kawaida Tofauti na Awali.
Media Wire Express, Imezungumza na Raphael Un’gen’ge ambaye ni Daktari wa Wanawake Katika Hospitali ya Rufaa Mkoa Mwananyamala, Juu ya Kuwepo kwa Matumizi Holela ya Madawa Yakuongeza Makalio, Pamoja Na Matiti Na nini Hasara zake Pamoja na Njia sahihi Yakufanya Hasa Kwa Wale Wanao Hitaji Kuongeza Makalio Au Matiti.
Daktari Amesema, Tanzania Imeanza Kupitia Tatizo hili Hasa Miaka Ya Karibuni ,Kutokana na Ukuaji Wa Teknolojia, Huku Wanawake Walio wengi Wakihitaji Kukimbizana Na Kasi Ya Ulimwengu
More On: Mad Rush for Hips/Butt Enhancing Procedures -Women Go “Gaga”
https://mediawireexpress.co.tz/ma
Daktari Ameongeza Kuwa Kutokana na Utafiti Kwa Sasa, Mitaani kuna Dawa Za Aina tatu zinazouzwa Kwaajiri ya Shighuli Izi, Ikiwemo Silicon, Dawa Za Kichina Pamoja Na Dawa Za Kienyeji Ambazo Kiutalamu Hazikidhi Tafiti za kisanyansi kwa Matumizi Ya Binadamu.
Madawa Haya Yanamadhara Makubwa Kwenye Mwili wa Binadamu Kwani Tunapata Kesi Kuwa Watu wanapata Kansa, wengine Vidonge Vinawaathiri hadi Maungo Yao Walio kusudia Kuyaongeza Yanakuwa Katika Hali Mbaya na Hata Kupelekea Kupishana, mfano Kalio Moja Linakua Kubwa Kuliko Jingine, Hata Wengine Wanapata Kansa Ya Damu na figo Kufeli
“Nawashauri Wanawake wanaohitaji Kuongeza au Kupunguza Makalio Yao, Wafanye Oparesheni ,Tena Kwa Bahati Nzuri ,Hospitali Yetu ya Mloganzila Sasa ,Wanafanya Upasuaji Huo,Tena Wanamadaktari Walio wabobezi Na Makini,
Hii ni Njia Bora Kuliko Kunywa Madawa Yatayo Hatarisha Mwili Wako”