Dark
Light

Lori la Mafuta Lapata Ajali Sekenke

Lori la mafuta lenye namba za Usajili T 851 APZ limeteketea Kwa moto katikati ya Mlima Sekenke, Mkoani Singida na kusababisha foleni kubwa ya magari yanayofanya safari zake kati ya Singida na Mkoa wa Tabora kupitia Igunga ambayo yamekwama kwa zaidi ya nusu saa, kufuatia lori hilo kugonga kingo za Mlima huo na kushika moto.
May 12, 2024
by
Lori la mafuta lenye namba za Usajili T 851 APZ limeteketea Kwa moto katikati ya Mlima Sekenke, Mkoani Singida na kusababisha foleni kubwa ya magari yanayofanya safari zake kati ya Singida na Mkoa wa Tabora kupitia Igunga ambayo yamekwama kwa zaidi ya nusu saa, kufuatia lori hilo kugonga kingo za Mlima huo na kushika moto.
Kwa mujibu wa mashuhuda, lori hilo liligonga kingo za barabara na kuanza kuteketea huku mafuta yakimwagika, jambo lililozua taharuki kubwa kwa watumiaji wa barabara hiyo.
Akiongea katika eneo la tukio hilo Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Selemani Mwenda amesema hakuna madhara yoyote yaliyotokea Kwa Binadamu na jitihada za kuwasiliana na Jeshi la Zimamoto Wilayani Igunga zimefanyika ili kurejesha mawasiliano ya barabara baina ya Mikoa hiyo miwili.
DC Mwenda alifika katika eneo hilo muda mfupi baada ya ajali hiyo kutokea akiwa ameambatana na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi CCM, Ally Hapi wakati wakiwa njiani kutoka Singida kuelekea mkoani Tabora kuhitimisha ziara ya Hapi ya Mikoa minne.

8 Comments

  1. Thanks a bunch for sharing this with all people you really recognise what you’re talking approximately! Bookmarked. Please additionally visit my site =). We may have a link change arrangement among us!

  2. After study a few of the blog posts on your website now, and I truly like your way of blogging. I bookmarked it to my bookmark website list and will be checking back soon. Pls check out my web site as well and let me know what you think.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Don't Miss

Zambia Enforces Electricity Rationing in Response to Drought Emergency

Zambia has announced it will start rationing its electricity, as

Trump Changed His Speech After Escaping Death

Former President of the United States Donald Trump has arrived