Meneja wa habari na mawasiliano wa Simba SC Ahmed Ally ametangaza kaulimbiu Yao Vita ya Kisasi kuelekea mchezo wao wa marudio dhidi ya Jwaneng Galaxy Machi 2
Ahmed amesema mchezo huo utakuwa wa kisasi dhidi ya mpinzani wao ili kuondoka na alama 3 za kuduzu hatua ya robo fainali.
“Tumezoea kwenda robo fainali, kwahiyo ni lazima tutinge robo fainali. Na hili inapaswa kufanyika kwa pamoja.” Amesema Ahmed.
Simba wapo kundi B la CAFCL, wakiwa nafasi ya pili kwa alama 6 wakifungana na Wydad AC walio nafasi ya tatu. Galaxy wanaburuza mkia wakiwa na alama 4 huku Asec Mimosa vinara wa kundi wakiwa na alama 11 huku wakiwa tayari wameshafuzu hatua ya robo fainali.
“Mechi dhidi ya Jwaneng Galaxy itachezwa Jumamosi Machi 2, 2024 saa 1:00 usiku. Licha ya mapendekezo yetu kucheza mechi saa 10:00 jioni lakini CAF wameamua iwe saa 1:00 usiku ili michezo yote iwe muda mmoja”.amesema Ahmed Ally.