Breaking News
Breaking News
Dark
Light

Davido vs. Wizkid: Mizozo Yawasha Moto Mtandaoni

Davido na Wizkid, ambao ni wasanii wenye umaarufu mkubwa na wafuasi wengi duniani kote wakiwa moja kati ya wasanii walioanza kutengeneza rekodi mbali mbali za ushirikiano na wasanii wa nje ya mipaka ya Nigeria hususani wasaniii wa marekani, pamoja na kujaza Viwanja vikubwa vya Nchi mbali mbali za Afrika na hata nje ya mipaka ya Afrika, wamekuwa wakichukuliwa kama wapinzani na mashabiki wao wamejigawa kuwa "Team Wizkid" na "Team Davido".
April 30, 2024
by

Kama ilivyo siku zote mafahari wawili kushindwa kukaa Zizi moja ndivyo ilivyo kwa Nyota wawili  wa Muziki kutoka Nchini Nigeria,Davido na Wizkido ambao uhusiano na ukaribu wao umekuwa ni wa kupanda na kushuka kwa takribani muongo mmoja sasa ambapo leo April 30 wamezua utata mkubwa kwenye mtandao wa kijamii wa X baada ya kushambuliana kwa maneno makali.

Davido na Wizkid, ambao ni wasanii wenye umaarufu mkubwa na wafuasi wengi duniani kote wakiwa moja kati ya wasanii walioanza kutengeneza rekodi mbali mbali za ushirikiano na wasanii wa nje ya mipaka ya Nigeria hususani wasaniii wa marekani, pamoja na kujaza Viwanja vikubwa vya Nchi mbali mbali za Afrika na hata nje ya mipaka ya Afrika, wamekuwa wakichukuliwa kama wapinzani na mashabiki wao wamejigawa kuwa “Team Wizkid” na “Team Davido”.

Read More:Davido’s hopes dashed as all 3 nominations yield no wins

Mvutano huo ulianza baada ya mashabiki kumtaka Wizkid kuachia wimbo mpya kwenye X. Badala ya kukubali ombi hilo, Wizkid aliweka video yenye utata ya Davido na kuandika, “Niombe hivi, nitume video.”

Miezi kadhaa iliyopita, video ilisambaa mitandaoni ikimwonyesha mtu anayefanana na Davido akionekana kuomba msaada. Davido, mwenye umri wa miaka 31, alijibu kwa kusema hatajishughulisha na mtu ambaye kazi yake ilipotea kabla ya kufufuka kwa muda mfupi tu, kama jibu kwa chapisho la Wizkid.

Hata hivyo, mashabiki wa wawili hao wamekuwa wakijitokeza kuwatetea wasanii wao, na mjadala huo umeendelea kuwasha moto. Kituo maarufu cha muziki cha Hip TV kimeanzisha kura ya maoni kwenye X ili kuamua ni nani kati ya Davido na Wizkid ameshinda vita hivyo.

Davido na Wizkid wote wawili wanachukuliwa kuwa nyota wakubwa wa muziki barani Afrika. Wamefanikiwa kushinda tuzo nyingi za muziki za kimataifa, ikiwa ni pamoja na tuzo za MTV na BET, na pia wameshirikiana na wasanii maarufu kama Drake, Chris Brown, na Nicki Minaj.

Mvutano huu kati ya Davido na Wizkid umekuwa ukigonga vichwa vya habari na kuendelea kuwasisimua mashabiki wa muziki nchini Nigeria na kote duniani.

Author

19 Comments

  1. I’m amazed, I have to admit. Rarely do I come across a blog that’s both educative and entertaining, and without a doubt, you’ve hit the nail on the head.
    The issue is something not enough people are speaking intelligently about.
    I’m very happy that I stumbled across this in my hunt for something concerning this.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Don't Miss

Ronaldo Asifiwa kwa Uchezaji Usio wa Ubinafsi na Martinez

Katika mechi ya hivi karibuni dhidi ya Uturuki, Cristiano Ronaldo

Tanzania Unveils Major Reforms to Improve Education Standards

Tanzania is taking bold steps to address long-standing issues in