Breaking News
Breaking News
Dark
Light

Wasichana 178,114 Kupatiwa Chanjo Mlango Wa Kizazi Singida

Mratibu huyo wa Chanjo amesema chanjo ya Mlango wa Kizazi - HPV- inafaida kubwa ikiwemo kutoa kinga kwa wasichana kutopata virusi vya saratani mbalimbali ikiwemo ya mlango wa kizazi.
April 16, 2024
by

Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe. Halima Dendego, amewahimiza Viongozi wa Serikali na wa Dini katika ngazi zote kuanza kampeni ya kuhamasisha wazazi kuwapeleka wasichana wenye umri wa kati ya miaka 9 hadi 14 kwenda kupata chanjo ya mlango wa kizazi ili kuwaepusha kupata saratani hiyo ambayo imekuwa ikileta madhara makubwa katika kundi hilo.

Read more: Waziri Ummy Aongoza Wananchi Matembezi Ya Afya

https://mediawireexpress.co.tz/waziri-ummy-aongoza-wananchi-matembezi-ya-afya/

Mkuu huyo wa Mkoa wa Singida ametoa kauli hiyo kwenye kikao kilichojumuisha Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, Viongozi wa Dini, Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa pamoja na Wataalamu wa Afya kutoka Wilaya zote za Mkoa huo.

Halima Dendego amesisitiza Wataalamu wa Afya Mkoani Singida kujipanga ipasavyo na kuweka mipango mizuri itakayosaidia wasichana lengwa wanapata chanjo hiyo bila kukosa Mijini na Vijijini.

Naye, Mratibu wa Huduma za Chanjo Mkoa wa Singida, Jadili Mhanginoma, amesema Serikali Mkoani Singida inatarajia kutoa chanjo hiyo kwa wasichana 178,114 wenye umri kati ya miaka 9 hadi 14 kuanzia Aprili 22 hadi 26 na kuendelea hadi Desemba mwaka huu.

Ameeleza kuwa kwa sasa tayari dozi 191,040 zimeshapokelewa na kusambazwa kwenye ngazi za Halmashauri mkoani Singida.

Read more: Wauguzi, Wakunga Wabeba Asilimia 60 Watumishi Sekta ya Afya

https://mediawireexpress.co.tz/wauguzi-wakunga-wabeba-asilimia-60-watumishi-sekta-ya-afya/

Mratibu huyo wa Chanjo amesema chanjo ya Mlango wa Kizazi – HPV- inafaida kubwa ikiwemo kutoa kinga kwa wasichana kutopata virusi vya saratani mbalimbali ikiwemo ya mlango wa kizazi.

Kwa Tanzania chanjo ya Mlango wa Kizazi – HPV- iliidhinishwa kuanza kutumika na Shirika la Afya Duniani kwa ushirikiano wa Wizara ya Afya kupitia Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba – TMDA – mwaka 2014 ambapo kwa mkoa wa Singida chanjo hiyo ilianza kutumika mwaka 2018.

Author

4 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Don't Miss

Tanzanian Local Elections Reflect Familiar Patterns Again

Tanzania’s recent local elections have sparked mixed reactions, with political

Congo Challenges China’s Hold on Cobalt Trade

The Democratic Republic of the Congo (DRC) is taking decisive