Breaking News
Breaking News
Dark
Light

Utajiri Wa Morogoro Upo Sekta Ya Kilimo – RC Malima

Uchumi wa Mkoa huo unapatikana katika sekta ya Kilimo kwa kuwa Mkoa huo una ardhi yenye rutuba, maji ya kutosha na hali ya hewa inayofaa kwa kilimo cha mazao karibu yote muhimu yanayolimwa hapa nchini.
March 28, 2024
by
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima amesema Uchumi wa Mkoa huo unapatikana katika sekta ya Kilimo kwa kuwa Mkoa huo una ardhi yenye rutuba, maji ya kutosha na hali ya hewa inayofaa kwa kilimo cha mazao karibu yote muhimu yanayolimwa hapa nchini.

Mhe. Malima amesema hayo Machi 26, 2024 wakati wa kongamano la Chemba ya Wafanyabiashara wa Viwanda na kilimo (TCCIA) lililofanyika Manispaa ya Morogoro likishirikisha watu mbalimbali wakiwemo wakulima, wafanyabiashara, wamiliki wa viwanda na taasisi za Kibenki.
Akizungumza katika kikao hicho Mhe. Malima amesema, ili Wakazi wa Morogoro waweze kukuza Uchumi wao, wanawajibika kuanza kulima kisasa kwa kuwa kwa sasa suala sio kulima pekee, bali kulima kulingana na uhitaji wa soko.

“Lazima tufanye kilimo cha uzalishaji chenye tija kinachoendana na uhitaji wa Soko la nchi zingine hususan Nchi ya India…” Amesema Malima.

Akizungumzia mahusiano baina ya Tanzania na India, mbele ya mwakilishi wa Balozi wa India hapa Nchini Bw. Manoj Verma Mkuu huyo wa Mkoa amebainisha umuhim wa Mkoa wa Morogoro kwenye mahusiano hayo kuwa yanatokana na utajiri wa Mkoa huo kwenye Sekta ya kilimo.

Amesema, kupitia mahusiano hayo, Mkoa wa Morogoro utanufaika kupitia Kilimo, kwa sababu India iko mbali kiteknolojia hivyo Tanzania wakiwemo wakazi wa Morogoro watapata ujuzi wa kilimo chenye tija kutoka India hususan kuzalisha mazao yao kwa wingi na kuboresha mazao hayo kulingana na masoko ya kimataifa.

Mhe. Malima amesema, mwaka 2024 Mkoa umejipanga kuzalisha miche milioni moja ya zao la mikarafuu na miche hiyo inatarajiwa kupandwa katika safu za milima ambayo imeharibiwa kutokana na shughuli za kibinadamu ikiwemo kukata mkaa, kuni pamoja na kilimo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa TCCIA Mkoa wa Morogoro Mwadhine Mnyanza amesema lengo la kongamano hilo ni kuboresha mahusiano baina ya Nchi ya India na Serikali ya Tanzania hususan Mkoa wa Morogoro na Sekta binafsi ili kujenga uelewa wa Pamoja na kuweka mikakati inayotekelezeka husuan katika sekta ya kilimo.

See translation

Author

6 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Don't Miss

No Citizen Stands Above Tanzanian Law, Says CCM Leader

The Vice Chairman of Tanzania’s ruling party on the mainland,

Israel Moves to Seize Full Control of Gaza City

Tensions in the Middle East have reached a critical point