Dark
Light

Mawasiliano Ya Barabara Ya Dar-Mtwara Yarejea

Mawasiliano ya barabara kuu ya kutoka Dar es Salaam na Mikoa ya Pwani, Lindi na Mtwara yarejea katika eneo la Somangafungu Mkoani Lindi kutokana na daraja la Somanga linalounganisha barabara hiyo kukatika na kusababisha barabara hiyo kufungwa kwa saa kadhaa.
March 25, 2024
by

Mawasiliano ya barabara kuu ya kutoka Dar es Salaam na Mikoa ya Pwani, Lindi na Mtwara yarejea katika eneo la Somangafungu Mkoani Lindi kutokana na daraja la Somanga linalounganisha barabara hiyo kukatika na kusababisha barabara hiyo kufungwa kwa saa kadhaa.

Akitoa taarifa, Kaimu Meneja wa TANROADS Mkoa wa Lindi, Eng. Emil Nzengo amesema tayari magari ya abiria na mizigo na vyombo vingine vya usafiri vimeruhusiwa na kuaza kupita upande mmoja katika Daraja hilo ambalo lilikuwa halipitiki tangu usiku wa kuamkia leo kutokana na mvua zinaoendelea kunyesha Mkoani humo.

“Tumekamilisha kazi awamu ya kwanza, wananchi na magari wameruhusiwa kuanza kupita. Tunawashukuru Wananchi kwa uvumilivu na tunaomba waendelee kuiamini Serikali ipo kazini kwa ajlili yao”, amesema Eng. Nzengo.

Awali, Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa alieleza kuwa jitihada kubwa zinaendelea za kurudisha mawasiliano ya barabara eneo la Somangafungu na kuagiza timu ya Wataalam kutoka TANROADS kuhakikisha hadi kufikia mchana leo March 25, 2024 mawasiliano yawe yamerejeshwa na magari yaanze kupita katika daraja hilo.

Author

4 Comments

  1. I am really impressed with your writing skills as well as with the layout on your blog. Is this a paid theme or did you customize it yourself? Either way keep up the nice quality writing, it’s rare to see a great blog like this one today..

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Don't Miss

EAC Ministers Agree to Accelerate Regional Integration

Ministers responsible for East African Affairs in the member states

Maelezo Ya  Mwisho za Rais Magufuli,CDF Mabeyo Afunua Siri ya Kifo Chake

Katika mahojiano na aliyekuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF),