Breaking News
Breaking News
Dark
Light

LAAC Imetoa Miezi 3 Ujenzi Kituo Cha Afya Bulela

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), Mheshimiwa Staslaus Mabula ametoa miezi 3 kwa Halmashauri ya Mji wa Geita kuhakikisha inakamilisha ujenzi wa Kituo cha Afya cha Bulela kilichopo katika Kata ya Bulela mkoani Geita.
March 20, 2024
by

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), Mheshimiwa Staslaus Mabula ametoa miezi 3 kwa Halmashauri ya Mji wa Geita kuhakikisha inakamilisha ujenzi wa Kituo cha Afya cha Bulela kilichopo katika Kata ya Bulela mkoani Geita.

Hayo yametolewa na  Makamu Mwenyekiti LAAC, Mheshimiwa Staslaus Mabula wakati wa majumuisho ya ziara ya Kamati  hiyo wakati wa  kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Halmashauri ya Mji wa Geita, mkoani Geita.

Amesema kuwa kituo hicho kitaendelea kutoa huduma huku kikiendelea kufanyiwa marekebisho mbalimbali ikiwemo kubadilisha sakafu na milango ambayo haina ubora.

Mabula pia ameishauri Halmashauri hiyo kutenga fedha kwa ajili ya ununuzi wa vifaa na vifaa tiba ili kituo hicho kinapokamilika kiweze kuwa na vifaa vitakavyoweza kutoa huduma bora kwa jamii

Pia imependekeza chumba cha upasuaji kikamilishwe kwa wakati na kutenga fedha za mapato ya ndani kwa ajili ya ununuzi wa vifaa ili kuanza kutoa huduma za upasuaji kwa mama wajawazito.

“Chumba cha upasuaji ni eneo muhimu sana kwa kuwa huko ndipo tunapowalenga wamama wajawazito wenye changamoto kupata matibabu hivyo hakikisheni inakamilika na vifaa vinakuwepo,” amesisitiza Mabula.

Aidha, Mabula amewataka kuhakikisha wanajibu hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) pamoja na za kamati ili kuzifuta na kuziondoa kabisa.

Author

3 Comments

  1. Howdy just wanted to give you a quick heads up. The text in your article seem to be running off the screen in Internet explorer. I’m not sure if this is a formatting issue or something to do with internet browser compatibility but I figured I’d post to let you know. The layout look great though! Hope you get the issue solved soon. Kudos

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Don't Miss

President Samia Arrives for SADC Summit

The Chairperson of the Southern African Development Community (SADC) Organ

Brazil Takes BRICS Leadership Amid Global Shifts

As global power dynamics continue to evolve, Brazil has assumed