Dark
Light

Serikali kujenga shule kila kijiji na vitongoji vikubwa

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema ni mkakati wa Serikali ya awamu ya sita kujenga shule kwenye kila kijiji na vitongoji vikubwa, amezungumza leo Februari 26, 2024 wakati wa ziara ya kikazi Bunda mkoani Mara.
February 26, 2024
by

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema ni mkakati wa Serikali ya awamu ya sita kujenga shule kwenye kila kijiji na vitongoji vikubwa, amezungumza leo Februari 26, 2024 wakati wa ziara ya kikazi Bunda mkoani Mara.

“Serikali ya awamu ya sita inawapenda watanzania wote ndio maana Rais wetu Dkt. Samia anatekeleza miradi mbalimbali ya maeneo katika sekta zote za maendeleo kuanzia ngazi ya Taifa hadi vijijini” Majaliwa

Hata hivyo Mhe. Majaliwa amesema kuwa Serikali ni imara na ina nia ya dhati ya kuendelea kuwatumikia watanzania kwa kufikisha maendeleo kwenye sekta zote za huduma za jamii katika kila eneo nchini

Pia ameeleza kuwa Sekta ya mifugo ni maisha na ni uchumi ndio maana Serikali imeanza na inaendelea na uratibu wa mpango wa kuwa na viwanda vya mazao ya mifugo

“endeleeni kufuga na mzingatie masharti ya ufugaji ili muweze kukuza uchumi wenu” amesema.

Author

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Don't Miss

Equatorial Guinea Restricts WhatsApp Amid Scandal Fallout

Equatorial Guinea has taken measures to block the use of

Ngassa Amjibu Mayele Yanga Kufuga Majini

Mchezaji wa zamani wa klabu ya Yanga Mrisho Ngassa ameposti