Watu 11 wamefariki dunia na wengine wawili kujeruhiwa baada ya mfumo wa joto wa kiwanda cha kuzalisha sukari cha Mtibwa kulipuka wakati wakijiandaa kuanza uzalishaji wa sukari kwenye kiwanda hicho kilichopo Turiani mkoani Morogoro.
Akizungumza na Media Wire Express leo Alhamisi Mei 23, 2024, Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Morogoro, Shaban Marugujo amesema mlipuko huo ulitokea saa 7 usiku na umeua watu 11 na wengine wawili kujeruhiwa.
“Ni kweli watu 11 wamefariki dunia na wengine wawili kujeruhiwa baada ya mlipuko wa mpira wa joto wakati wanajiandaa na uzalishaji wa sukari pale kiwandani.
Ifahamike ili sukari ichakatwe kuna kiwango cha joto ambacho kinatakiwa kifikie, sasa wakati maandalizi ya uzalishaji yakifanyika na kile kiwango cha joto kikingojewa ndipo ukatokea mlipuko huo na kuwakuta watu hao 11 ambao kwa kiwango kile cha joto wakafariki papo hapo,” amesema Marugujo.
Amesema:”Chanzo halisi cha mlipuko huo bado hatujakipata ila bado tunaendelea na uchunguzi, timu nzima iko hapa kiwandani tangu usiku huo na mpaka sasa tunaendelea na tukikamilisha tutatoa taarifa rasmi.”
Thank you a lot for giving everyone such a breathtaking opportunity to check tips from this site. It is often very good plus stuffed with a good time for me personally and my office acquaintances to search your site a minimum of 3 times in 7 days to read the new guidance you have got. Not to mention, we are usually astounded with your tremendous things you serve. Selected 4 ideas in this article are certainly the simplest I have ever had.
Loving the info on this web site, you have done outstanding job on the content.