Mkurugenzi wa Taasisi ya Wajibu Ludovick Utouh amesema katika tukio la sauti za waandishi kuwa “ ni ngumu kukomesha rushwa kwa waandishi wa habari kwa sababu hawalipwi vizuri”leo Februari 16 jijini Dar es Salaam.
“Baadhi ya vyombo vya habari vina hali ngumu ya kiuchumi ili kumuwezesha muandishi kwenda sehemu ya tukio ambapo ni mbali na eneo lake kwa lengo la kutimiza wajibu wake, lakini endapo atachukua pesa hiyo kama sehemu ya ulaghai wa kuandika mazuri ya aliyemtuma basi hiyo itakuwa rushwa.”Amesema Utouh
Mkurugenzi huyo alitoa maoni hayo baada ya swali kutoka kwa mdau Benedict Mrema kuuliza “je kuna ubaya muandishi wa habari kupewa pesa ya kwenda kufata habari mbali na eneo lake kama sehemu ya kumuwezesha kufanya kazi kwa usahihi?”
Pia Fausta Msokwa amesema muandishi wa habari kupewa bahasha ni tatizo kwa namna yoyote ile kwasabubu itamfanya aegemee upande mmoja ili siku nyingine asikose kuwezeshwa wakati wa utoaji taarifa.