Breaking News
Breaking News
Dark
Light

Fainali ya CCC Yawaangukia Waarabu

Utamu wa fainali hii unakolezwa na matokeo ya nusu fainali ya Michuano hii Msimu Uliopita ambapo Timu hizi zilikutana na Ahly Kuibuka Mbabe na kusonga katika hatua ya fainali amabapo walitwaa Ubingwa wa kombe hilo mbele ya Wydad Casablanca ya Nchini Moroco, Je Esperance atalipa kisasi, Au Ahly ataendeleza Ubabe? Ni swala la muda tu.
April 27, 2024
by

Wahenga walipo sema waarabu wa pemba wanajuana kwa vilemba hawakukosea na Aijuae njia katu hapotei, Fainali ya Vilabu Bingwa Afrika Itawakutanisha Timu ya karne kutoka Misri @alahly na Miamba kutoka Tunisia @esperance_sportive_detunis na hii ni baada ya timu zote kufuzu katika mchezo wa nusu Fainali ya mkondo wapili ambapo Ahly walipepetana na TP mazembe ya Congo DR hapo jana ikiwafunga Mabao matatu kwa Mtungi Huko MIsri, Huku Esperanse Wakiwavurumusha Mamelodi Sundowns Kwa Matekeo ya Jumla ya goli mbili kwa bila.

Ikumbukwe timu hizo mbili kutoka kaskazini mwa Afrika ndizo timu pekee zilizo fuzu hatua ya Robo fainali ya michuano hiyo, huku wengi waakizipa nafasi timu ya Mamelodi Sundowns na Petro Atletico De Luanda Ya Angola kutinga Fainali kutokana na kufanya vizuri katika hatua za makundi.

Read More:Yanga SC Yatuma Malalamiko CAF Kudhulumiwa Goli

Mnzani umeelemea Upande mmoja na kudhihirisha utawala wa timu kutoka kaskazini mwa Afrika kuendeleza Ubabe wa soka la Afrika kwa kucheza fainali nyingi za Michuano hiyo na Kuchukua makombe mengi.

Utamu wa fainali hii unakolezwa na matokeo ya nusu fainali ya Michuano hii Msimu Uliopita ambapo Timu hizi zilikutana na Ahly Kuibuka Mbabe na kusonga katika hatua ya fainali amabapo walitwaa Ubingwa wa kombe hilo mbele ya Wydad Casablanca ya Nchini Moroco, Je Esperance atalipa kisasi, Au Ahly ataendeleza Ubabe? Ni swala la muda tu.

Tayari Ratiba za CAF juu ya Mechi hizo za Fainali zimewekwa wazi, ambapo Mkondo wa kwanza Utafanyika katika Mji wa Rades huko Tunisia Mnamo May 18, wakati Mkondo wa pili utachezwa May 25  kwa mafarao huko Cairo, Misri.

Endapo Ahly atachukua Kombe hili itakuwa ni mara ya pili mfululizo akitwaa taji hilo na kuendelea kusimika rekodi yake ya kua klabu yenye makombe mengi Afrika Akiwa na idadi ya makombe 11 ya ligi ya mabingwa Afrika hadi sasa, huku Esperance wakitwaa Ubingwa huo kwa Mara ya mwisho mwaka 2019.

Author

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Don't Miss

Karioko Building Collapse Death Toll Rises To 13

The death toll form the karioko buiding collapse has risen

Tanzania and Ethiopia Seal Trade Deals

Tanzania and Ethiopia this week signed bilateral agreements targeting agriculture,